Na MatukiodaimaBlog
WANAFUNZI waliosoma shule
ya sekondari Ilula wilayani Kilolo mkoa wa Iringa wametoa msaada
wa fedha kiasi cha Tsh milioni 1.3 kwa ajili ya kuchangia
ukarabati wa shule hiyo baada ya kukumbwa na maafa ya kuezuliwa na
kimbuka vyumba vya madarasa na bweni la wanafunzi.
Wakikabidhi
maasada huo mchungaji Yekonia Koko na Mwalimu Nguvu Chengula
jana kwa niaba ya umoja wa wanafunzi waliosoma katika shule
hiyo walisema kuwa wameguswa na changamoto mbali mbali zilizopo
katika shule hiyo hasa baada ya kupatwa na maafa ya vyumba vya
madarasa na bweni kuezuliwa na kimbunga na kupelekea wanafunzi
kuendelea kulala darasani kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.
Hivyo
walisema kupitia umoja wao wanafunzi waliosoma katika shule
hiyo wamelazimika kuchangishana fedha ili kusaidia uboreshaji
wa shule hiyo kama sehemu ya mchango wao kwa shule hiyo pia
njia moja wapo ya uhamasishaji wa wananchi kuendelea kuchangia
maendeleo ya elimu badala ya kuiachia serikali .
Alisema Chengula
kuwa baada ya serikali kufuta ada katika shule ya msingi na
sekondari wananchi wanao wajibu wa kushiriki kuchangia maendeleo ya
shule hiyo kama ujenzi na ukarabati wa shule kwani pasipo
kufanya hivyo shule nyingi zitabaki magofu kutokana na baadhi ya
wananchi kuwa na dhana potofu kuwa hawapaswi kuchangia maendeleo
ya elimu .
Chengula
ambae ni mkurugenzi wa shule ya Sun Academy mjini Iringa alisema
kuwa ili jamii iweze kunufaika na ubora wa elimu inayotolewa
nchini ni lazima mazingira ya ufundishaji na mashule kuboreshwa
na njia pekee ya kuboresha ni pamoja na wananchi kuendelea kutoa
ushirikiano kwa uongozi wa shule ikiwa ni pamoja na kuwa na harambee
za mara kwa mara kwa ajili ya kuboresha majengo ya shule .
"
Shule hii hii imetoa wanafunzi wengi sana ambao baadhi yao kwa
sana wanafanya kazi katika maeneo mbali mbali na baadhi yao
wameanzisha shule zao binafsi kama ilivyo kwangu mimi .........ila
shule hizi ambazo zimetuwezesha hadi kufika hapa zina changamoto
nyingi zikiwemo za uchakavu wa majengo jukumu letu ni kurudisha
shukrani kwa shule tulizosoma kwa kuchangia maendeleo ya shule
hizi ili wanafunzi wasome katika mazingira mazuri zaidi"
Hata
hivyo alisema inasikitisha kuona wanafunzi wanaendelea kulala
darasani kutokana na bweni lao kuezuliwa na kimbunga na kuwa kuna haja
ya serikali ya wilaya ya Kilolo na wadau kufanya jitihada za
kuboresha miundo mbinu ya bweni hilo ili kuwawezesha wanafunzi
kurejea katika bweni badala ya kuendelea kulala darasani.
Kuhusu
wanafunzi waliosoma katika shule hiyo na sasa wanafanya kazi
katika taasisi na wengine kuwa na taasisi zao aliwataka kukutana
na kuangalia uwezekano wa kupeana majukumu ya kuchangia uboreshaji
wa shule hiyo kama ambavyo wachache wao walivyoanza kuchangia
kwa ajili ya uboreshaji wa shule hiyo.
Wakati
mchungaji Koko alieleza kusikitishwa kwake na miundo mbinu mibovu
ya umeme iliyopo katika shule hiyo na kuwa pasipo shirika la umeme
nchini (Tanesco) wilaya ya Kilolo na mkoa wa Iringa kuchukua
jitihada za haraka upo uwezekano wa shule hiyo kukumbwa na maafa
siku za mbeleni .
Kwani
alisema inasikitisha kuona nguzo ambazo zimepeleka umeme katika
mabweni ya wanafunzi kuwa za kienyeji ambazo zimewekwa na uongozi wa
shule hiyo na umeme unaotumika shuleni hapo kuwa umeme wa kiwango
cha chini zaidi baada ya kuwekewa umeme wa njia mbili badala ya njia
tatu ambao umewezesha shule hiyo kuwa na uhakika wa umeme.
Mkuu
wa shule hiyo Vecent Shauri mbali ya kuwashukuru wanafunzi hao
waliopata kusoma katika shule hiyo kwa kusaidia kiasi hicho cha
fedha kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo bado alisema tayari
uongozi wa shule hiyo ulijaza fomu TANESCO kuomba kufikishiwa
umeme wa uhakika na kuwa ni nguzo tatu pekee zinahitajika ila hadi
sasa zaidi ya miaka mwaka mmoja hawajafika kusogeza umeme katika
shule hiyo.
Akitoa
taarifa ya uchakavu wa majengo ya shule hiyo alisema kuwa
jitihada mbali mbali zimefanyika hasa baada ya shule hiyo kuezuliwa
na kimbunga na kuwa jitihada za wadau mbali mbali zimefanyika
kukabati vyumba vya madarasa vilivyoezuliwa japo alisema hadi sasa
bweni moja bado kukarabatiwa hivyo wanafunzi wanaendelea kulala
darasani.
|
No comments:
Post a Comment