BIASHARA ya maboga yenye mbegu yashika kasi katika migahawa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa baada ya baadhi ya wanaume kupenda kutumia maboga yenye Mbegu kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume.

Mtandao wa matukiodaimablog umebaini hali hiyo leo katika migahawa iliyopo nje ya ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kwa wanaume wanaofika kugombea maboga yenye mbegu kuliko vitafuno vingine.

Mfanyabiashara wa mgahawa eneo hilo Raha Juma Mlula anasema kuwa maboga yamekuwa yakiisha mapema kuliko maandazi ama vitafuno vingine na wateja wakikosa maboga husikitika zaidi.

Hata hivyo alisema kipande cha boga huuzwa Tsh 500 wakati chapati na maandazi ni Tsh 300 ila wengi hukimbilia maboga

Alisema boga moja kwa wakulima wananunua Tsh 1500 na wao hupata Tsh 3000 baada ya kuuza.

 Alisema kuwa kwa sasa upatikanaji maboga ni wa shida kutokana na watu wengi kupenda kutumia maboga wakati wa kunywa chai asubuhi.

" Wengi wanakula ni wanaume ambao wanaimani kuwa zinasaidia kuongeza nguvu za kiume…. Ila mimi najua mbegu za maboga zinazosaidia kuongeza nguvu za kiume au za kike ni zile mbichi zisizopikwa"

Habari zaidi utaipata baada ya kumpata mtaalam wa Afya