Friday, 24 February 2017 04:01

NIZUSHI MTUPU KUHUSU AFYA YA MZEE MWINYI



Image result for mwinyi Rais
 Kumekuwa na habari zinazoenea na kujirudia sana katika mitandao ya kijamii kuhusu hali ya afya ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Alli Hassan Mwinyi. Taarifa hizo ambazo hazieleweki lengo lake, zimekuwa zikidai kuwa Mzee Mwinyi amefariki dunia.
Tutautaarifu umma kuwa habari hizo si za kweli, ni za kupuuzwa. Mzee Mwinyi ni mzima wa afya, anaendelea na majukumu yake kama kawaida ambapo jana Alhamisi amehudhuria chakula cha jioni kuadhimisha siku ya Taifa la Kuwait na leo mchana alitarajiwa kwenda kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya.
Natumia fursa hii kuendelea kuwakumbusha watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa waliobuni teknolojia hii walikuwa na malengo adhimu ya kumpatia mwanadamu uwanja na uwanda mpana wa mawasiliano-tusiwachezee shere wabunifu hao kwa kuitumia kinyume cha malengo.
Aidha, jamii ifahamu kuwa ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni, 2015, kwa mtu yeyote kutangaza, kuchapisha au kueneza habari za uongo au uzushi katika mitandao.
Kwa niaba ya Serikali nachukua fursa hii kuwapa pole familia ya Mzee Mwinyi na watanzania wengine kwa mshtuko walioupata kutokana na uzushi huu. Katika hili hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika kuhusika na uhalifu huu.
 
 Dkt. Hassan Abbasi
Mkurugenzi, Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali

 Dar es Salaam, Ijumaa, Februari 24, 2017: 

TPDC YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI MIKOA YA IRINGA ,NJOMBE NA RUVUMA

WANAFUNZI WALIOSOMA ILULA SEKONDARI WACHANGIA PESA ZA UKARABATI WA SHULE


Wawakilishi wa  wanafunzi  waliosoma  shule ya  sekondari  Ilula  katika  wilaya ya  Kilolo  mkoani  Iringa Mwalimu  Nguvu  Chengula  kushoto na mchungaji  Yekonia Koko  wakimkabidhi  fedha  kiasi cha  Tsh  milioni 1.3 mkuu wa  shule ya  sekondari  Ilula mwalimu  Vincent  Shauri (katikati)  kulia ni makamu  mkuu wa  shule  hiyo  Joachim Mlay
Mkuu  wa  shule ya  Sekondari  Ilula  katikati  akiwaonyesha  choo  cha  kisasa  kinachojengwa  shuleni hapo kwa  ajili ya matumizi ya  walimu
Mkuu  wa  shule ya  Sekondari  Ilula  Vicent Shauri  kulia  akionyesha  choo  hicho
Hiki  ndicho  choo cha  walimu  kinachojengwa  shule ya  sekondari  Ilula
   hizi  ndizo  nguzo  za  umeme  zinazoelekea  bwenini  kweli  serikali  Kilolo  kuna haja ya  kulitazama  hili  kabla ya  kuleta  majanga
Mkuu  wa shule ya  sekondari  Ilula akionyesha  nguzo za  umeme
Bweni  lililoezuliwa na kimbunga  likiwa bado  kuezekwa
Na  MatukiodaimaBlog
WANAFUNZI  waliosoma   shule ya  sekondari  Ilula  wilayani  Kilolo  mkoa wa  Iringa wametoa  msaada  wa  fedha  kiasi cha  Tsh milioni 1.3  kwa ajili ya  kuchangia ukarabati  wa shule   hiyo baada ya  kukumbwa na maafa ya kuezuliwa na  kimbuka  vyumba  vya  madarasa na bweni la  wanafunzi.

Wakikabidhi  maasada huo    mchungaji  Yekonia Koko na Mwalimu  Nguvu  Chengula jana  kwa niaba ya  umoja  wa  wanafunzi  waliosoma  katika   shule   hiyo  walisema kuwa  wameguswa na  changamoto  mbali mbali  zilizopo  katika shule  hiyo  hasa  baada ya  kupatwa na maafa ya  vyumba  vya  madarasa  na bweni kuezuliwa na  kimbunga  na  kupelekea  wanafunzi  kuendelea  kulala darasani  kwa  zaidi  ya  mwezi mmoja  sasa.

Hivyo  walisema  kupitia  umoja   wao wanafunzi  waliosoma katika   shule  hiyo  wamelazimika  kuchangishana   fedha  ili  kusaidia  uboreshaji  wa  shule   hiyo kama sehemu ya  mchango  wao kwa  shule  hiyo  pia   njia  moja wapo ya uhamasishaji wa  wananchi kuendelea  kuchangia  maendeleo ya  elimu badala ya  kuiachia  serikali .

Alisema Chengula  kuwa baada ya  serikali  kufuta ada  katika  shule ya  msingi na  sekondari  wananchi  wanao wajibu wa  kushiriki kuchangia maendeleo ya  shule  hiyo  kama  ujenzi na ukarabati  wa  shule kwani  pasipo  kufanya    hivyo shule  nyingi  zitabaki magofu kutokana na baadhi ya wananchi   kuwa na dhana  potofu  kuwa hawapaswi  kuchangia  maendeleo  ya  elimu .

Chengula  ambae ni mkurugenzi  wa  shule ya  Sun Academy mjini  Iringa alisema  kuwa ili  jamii  iweze  kunufaika na ubora  wa  elimu  inayotolewa  nchini ni  lazima  mazingira ya  ufundishaji  na mashule  kuboreshwa   na njia  pekee ya  kuboresha  ni pamoja na wananchi kuendelea  kutoa  ushirikiano kwa uongozi wa  shule ikiwa ni  pamoja na kuwa na harambee  za mara kwa mara kwa ajili ya  kuboresha majengo ya  shule .

" Shule   hii hii  imetoa  wanafunzi  wengi  sana ambao baadhi yao  kwa   sana  wanafanya kazi katika maeneo mbali mbali na baadhi yao  wameanzisha shule  zao binafsi kama ilivyo kwangu mimi .........ila shule  hizi  ambazo zimetuwezesha  hadi kufika  hapa  zina  changamoto nyingi  zikiwemo  za uchakavu wa majengo  jukumu  letu ni  kurudisha shukrani kwa  shule  tulizosoma kwa kuchangia maendeleo  ya  shule  hizi  ili  wanafunzi  wasome katika mazingira  mazuri  zaidi"

Hata  hivyo alisema  inasikitisha kuona  wanafunzi  wanaendelea  kulala  darasani  kutokana na bweni lao  kuezuliwa na kimbunga na kuwa kuna haja ya  serikali ya  wilaya ya  Kilolo na  wadau  kufanya  jitihada za kuboresha  miundo  mbinu ya  bweni hilo  ili  kuwawezesha  wanafunzi  kurejea katika  bweni  badala ya  kuendelea  kulala darasani.

Kuhusu  wanafunzi  waliosoma  katika  shule  hiyo na  sasa wanafanya kazi  katika taasisi  na wengine kuwa na  taasisi zao  aliwataka   kukutana  na  kuangalia  uwezekano wa  kupeana majukumu ya  kuchangia  uboreshaji wa  shule   hiyo  kama ambavyo  wachache   wao  walivyoanza kuchangia kwa  ajili ya uboreshaji wa  shule   hiyo.

Wakati  mchungaji Koko  alieleza  kusikitishwa  kwake na miundo  mbinu  mibovu ya  umeme iliyopo katika shule  hiyo na  kuwa  pasipo  shirika la umeme nchini (Tanesco)  wilaya ya  Kilolo na  mkoa  wa Iringa kuchukua  jitihada za haraka upo uwezekano  wa  shule  hiyo  kukumbwa na maafa  siku za  mbeleni .

Kwani  alisema inasikitisha  kuona nguzo  ambazo zimepeleka  umeme  katika mabweni ya  wanafunzi  kuwa za kienyeji  ambazo zimewekwa na uongozi wa  shule  hiyo na umeme  unaotumika  shuleni hapo  kuwa umeme wa kiwango  cha  chini  zaidi baada ya  kuwekewa umeme wa njia mbili badala ya njia  tatu  ambao  umewezesha  shule  hiyo  kuwa na uhakika  wa umeme.

Mkuu  wa  shule  hiyo  Vecent Shauri   mbali ya  kuwashukuru  wanafunzi hao  waliopata  kusoma katika  shule  hiyo  kwa  kusaidia  kiasi hicho  cha  fedha kwa  ajili ya  ukarabati wa  shule   hiyo  bado  alisema tayari  uongozi wa  shule   hiyo  ulijaza  fomu TANESCO  kuomba  kufikishiwa  umeme wa uhakika na kuwa ni nguzo tatu  pekee  zinahitajika  ila hadi  sasa zaidi ya  miaka  mwaka mmoja  hawajafika  kusogeza umeme katika  shule  hiyo.

Akitoa  taarifa  ya uchakavu  wa  majengo ya  shule  hiyo alisema  kuwa jitihada mbali mbali  zimefanyika hasa  baada ya shule   hiyo  kuezuliwa na kimbunga na kuwa  jitihada  za  wadau  mbali mbali  zimefanyika  kukabati  vyumba vya madarasa  vilivyoezuliwa japo  alisema  hadi  sasa bweni moja  bado  kukarabatiwa hivyo  wanafunzi wanaendelea  kulala darasani.

Wednesday, 22 February 2017 12:09

TPDC YATOA MAFUNZO KWA WANAHABARI NYANDA ZA JUU KUSINI KUHUSU GESI ASILIA


Wanahabari mkoa  wa  Iringa  walioshiriki  warsha ya siku  moja ya gesi asilia  wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya  Iringa Richard Kasesela wa  tatu  kutoka  kushoto na wawezeshaji wa  warsha hiyo  kutoka TPDC,warsha iliyofanyika  ukumbi wa  VETA  Iringa kwa  kushirikisha  wanahabari kutoka mkoa  wa  Njombe ,Ruvuma na wenyeji  Iringa
DC  Kasesela  akifungua  warsha hiyo

RIDHIWANI KIKWETE AKANUSHA KUHUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA

Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete amekanusha vikali shutuma zilizotolewa dhidi yake kuhusu kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Moja ya magazeti ya  wiki  yamechapisha habari inayomtaja mbunge huyo kujihuisha na bishara ya dawa za kulevya ambayo imekuwa ikipigwa vita kila kona ya nchi kutokana na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Gazeti hilo limeandika kuwa, jina la Ridhiwani limetajwa katika orodha ya watuhumiwa wa dawa za kulevya na kuwa uchunguzi utafanyika. Pia limesema mbunge huyo ametoa kauli nzito kwa hadhara.

Kiongozi huyo kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa, hafanyi biashara hiyo haramu wala hakuwahi kufikiria kuifanya na kwamba nafsi yake i tayari kufa masikini kuliko kupata utajiri kupitia njia hiyo.

Aidha, ameeleza kuwa, anaamini kwamba uchunguzi utafanywa ili kuweza kuweka mambo sawa kwani yeye hana kitu chochote cha kuficha. 

Amesema kwamba, maneno hayo ya shutuma juu yake ni ya uongo na kwamba yametolewa na watu wasiomtakia mema na wasio na haya.