Ikulu ya Marekani imesema Rais wa nchi hiyo Donald Trump anaweza kutoza
asilimia 20 ya kodi kwa bidhaa zinazoingizwa nchini humo kutoka Mexico
kuweza kusaidia mpango wa kujenga ukuta kati ya nchi hizo mbili kuzuia
kuingia kwa Wahamiaji haramu na madawa ya kulevya.
Mexico imesisitiza kuwa haitolipia gharama za ujenzi wa ukuta huo na
kwamba pendekezo hilo jipya lililotolewa litasababisha kuzidisha ufa wa
kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili na kusababisha Rais Enrique Pena
Nieto kufuta ziara yake ya kukutana na Rais Trump wiki ijayo mjini
Washngton.
Uamuzi wa Rais Pena Nieto umeungwa mkono nchini mwake, akiwemo pia mtangulizi wake Vicente Fox.Katika Hatua nyingine Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May atakuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na Rais Trump.
Katika ziara yake nchini Marekani tayari amekutana na wanachama wa Republican mjini Philadelphia ambapo amesema Uingereza na Marekani hazipaswi kurudi katika kile alichokiita sera za uvamizi zilizoshindwa, walizokuwa wakizitumia awali.
Hata hivyo amesema nchi hizo mbili bado zina jukumu la kuongoza dunia